Juni 02, 2026, Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, alipata heshima ya kuhudhuria Kikao cha 41 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la 13 kufuatia mwaliko kutoka kwa Mh. Asha Feruzi (MB), Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Vyuo na Vyuo Vikuu. Prof. Sanga aliambatana na baadhi ya viongozi wa Menejimenti ya TEWW, jijini Dodoma.