Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika kukuza elimu jumuishi, mbadala na endelevu, hususan kwa wananchi waliokosa fursa ya elimu katika mfumo rasmi. Prof. Mushi amesema hayo Disemba 17, 2025 jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya 64 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), akisisitiza kuwa maendeleo ya taifa yanategemea uwezeshaji wa wananchi kielimu, kiujuzi na kiakili. Prof. Mushi ameipongeza TEWW kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Programu ya Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu (IPOSA), pamoja na maboresho ya mitaala inayozingatia mafunzo ya amali, stadi za maisha, ujasiriamali na matumizi ya teknolojia.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imeandika historia nyingine kwa kufanya mahafali yake ya 64 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Desemba 17, 2025. Mahafali hayo yameelezwa kuwa kielelezo cha mafanikio ya juhudi za Serikali katika kukuza elimu jumuishi, mbadala na endelevu, hasa kwa wananchi waliokosa fursa ya elimu katika mfumo rasmi.
-
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Philipo Sanga, akizungumza na maafisa usafirishaji na mama lishe (hawapo pichani) katika mafunzo ya ujasiriamali, usalama barabarani, afya na mazingira, jijini Mbeya tarehe 12 Agosti 2025, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya taasisi hiyo.
Baadhi ya maafisa usafirishaji wakisikiliza kwa makini mafunzo ya usalama barabarani yanayotolewa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, jijini Mbeya tarehe 12 Agosti 2025, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mh. Solomon Itunda (katikati ya waliokaa), akiwa na Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Philipo Sanga (kulia kwake), katika picha ya pamoja na baadhi ya mama lishe, mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali, usalama barabarani, afya na mazingira, jijini Mbeya tarehe 12 Agosti 2025.
Mkuu wa TEWW, Prof. Philipo Sanga, akieleza shughuli za Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na mkakati wa kitaifa wa kisomo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mafunzo ya uendeshaji wa madarasa ya kisomo, Urambo - Tabora, Agosti 6, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Dkt. Khamisi Mkanachi (katikati), akikabidhi vitendea kazi kwa Bi. Huruma Mgoo ambaye ni mwalimu wa kituo cha kisomo Urambo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya uendeshaji wa madarasa ya kisomo Urambo – Tabora, Agosti 06, 2025. Huruma Daniel Mgoo
Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Dkt. Khamisi Mkanachi (aliyeketi katikati), akifuatiwa na Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Philipo Sanga (kulia kwa mgeni rasmi), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanufaika wa madarasa ya kisomo mkoani Tabora baada ya tukio la uzinduzi wa mafunzo ya uendeshaji wa madarasa ya kisomo, Agosti 6, 2025, Urambo–Tabora.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 17,2025 jijini Dodoma kuhusu maadhimisho hayo ambayo yanatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 25 Agosti,2025 na kufungwa Agosti 27,2025 na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko.
"Maadhimisho haya yenye kauli mbiu isemayo: "Elimu bila ukomo kwa maendeleo endelevu" yanalenga kuhuisha kasi ya wadau wa kitaifa na kimataifa ya kuendeleza elimu ya watu wazima nchini na kuongeza uelewa wa umma kwamba elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi ni nyenzo muhimu kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi", alisema Prof.Mkenda.
Amesema kuwa, maadhimisho hayo yanalenga kuangazia umuhimu mkubwa wa kujua kusoma na kuandika katika kuendelea kujifunza bila ukomo na kuamsha ari na hamasa miongoni mwa vijana na watu wazima ya kupata ujuzi katika masuala ya ujasiriamali na ufundi wa awali.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE) ilianzishwa mwaka 1960 kama kitengo cha masomo ya nje ya darasa cha Chuo cha Makerere, chini ya Chuo Kikuu cha London. Mnamo mwaka 1963, Taasisi hiyo iliboreshwa...