Dodoma, Juni 21, 2026: Wananchi kutoka maeneo mbalimbali wameendelea kutembelea Banda la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, kujifunza kuhusu huduma na programu mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo.