Juni 2, 2026, Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, kuhusu fursa za elimu na maendeleo ili kutatua changamoto ya ajira kwa vijana, jijini Dodoma.
Viongozi hao walikubaliana kuanzisha rasmi na kuimarisha ushirikiano kwa lengo la kuongeza fursa za elimu na maendeleo kwa vijana wa Tanzania na kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kujenga taifa lenye vijana wenye ujuzi na uwezo wa kujitegemea.