TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA
(TEWW)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
KONGAMANO LA SIKU YA KISOMO KIMATAIFA NA JUMA LA ELIMU BILA UKOMO
KONGAMANO LA SIKU YA KISOMO KIMATAIFA NA JUMA LA ELIMU BILA UKOMO
29th Sep, 2026

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) inaendelea kuimarisha fursa za elimu na ujifunzaji kwa wananchi kupitia Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, kwa lengo la kuwapatia maarifa, ujuzi na stadi zitakazowawezesha kujiendeleza, kujitegemea na kuchangia maendeleo ya familia, jamii na taifa.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Kimataifa na Juma la Elimu Bila Ukomo, Septemba 24, 2026 mkoani Simiyu, Mkuu wa TEWW, Prof. Philipo Sanga, ametoa msisitizo kwa Maafisa Elimu, Maafisa Elimu ya Watu Wazima na wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana katika kusimamia na kutekeleza programu za Elimu Bila Ukomo kwa ufanisi.

Amesisitiza umuhimu wa kuongeza ushiriki na kufikisha fursa za elimu kwa wananchi katika maeneo mbalimbali, ili kujenga jamii yenye utamaduni wa kujifunza na kutumia maarifa katika kuboresha maisha na kuleta maendeleo.

slot gacor