Leo, Agosti 3, 2026, Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, amekutana na ugeni kutoka Chuo Kikuu cha Bar-Ilan kutoka nchini Israel ulioongozwa na Prof. Michal Zion, kwa lengo la kujadiliana ushirikiano katika elimu, utafiti na kujenga uwezo wa walimu na wawezeshaji.
Katika mazungumzo hayo, Prof. Sanga amewasilisha vipaumbele vya Taasisi vinavyozingatia Mpango Mkakati wa TEWW na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku ushirikiano huo ukitarajiwa kuimarisha ubora wa elimu, kuongeza mwonekano wa TEWW kimataifa na kuendeleza agenda ya umataifaishaji wa elimu.