TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA
(TEWW)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
MAONESHO YA WIKI YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU
MAONESHO YA WIKI YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU
21st Aug, 2026

Wanufaika wa Mradi wa IPOSA wakitoa maelekezo kwa wananchi waliotembelea banda la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) katika Maonesho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, Jijini Tanga, Agosti 21, 2026.

‎Katika maonesho hayo, wanufaika wanaonesha bunifu mbalimbali walizozalisha kupitia ujuzi walioupata katika Mradi wa IPOSA unaofadhiliwa na UNICEF.

Bunifu hizo ni pamoja na Tanzania Road Intelligence (TRI), mfumo unaolenga kutumia taarifa za wakati halisi kuimarisha usalama barabarani; Caller Device, kifaa kinachotumia sensor kutoa taarifa kwa mmiliki pale mlango unapofunguliwa; Zapper Device, prototype ya utafiti inayochunguza matumizi ya mapigo maalum ya umeme katika kudhibiti bakteria;

‎Pamoja na jiko la nishati mbadala linalotumia oil iliyotumika, linalolenga kupunguza gharama za nishati ya kupikia na matumizi ya kuni na mkaa.

‎Bunifu hizo zinaonesha namna Mradi wa IPOSA unavyowawezesha vijana kutumia ujuzi na ubunifu kutengeneza suluhisho za changamoto mbalimbali katika jamii.

slot gacor