Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, Septemba 23, 2026 ametembelea Banda la TEWW katika Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Kitaifa na Juma la Elimu Bila Ukomo yanayofanyika katika Viwanja vya CCM, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, ambapo amekutana na wanufaika wa programu na miradi mbalimbali ya Taasisi hiyo, ikiwemo IPOSA, MUKEJA na SEQUIP-AEP.
Prof. Sanga amewapongeza wanufaika hao kwa kutumia fursa zinazotolewa kupitia programu na miradi hiyo, huku wanufaika hao wakieleza namna walivyonufaika na elimu, maarifa na stadi walizozipata, ambazo zimewasaidia kuongeza uwezo na kuboresha maisha yao.