Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Philipo Sanga, amewahimiza walimu kuendelea kuwekeza katika ubora wa ufundishaji na kujiendeleza kielimu ili kuongeza maarifa na uwezo wa kuwaandaa wanafunzi kuwa kizazi bora cha Watanzania. Amesisitiza kuwa mwalimu ni nguzo muhimu ya mafanikio ya elimu na kipimo cha aina ya kizazi kinachoandaliwa.
Prof. Sanga ameyasema hayo leo Agosti 28, 2026 katika Mahafali ya Tano ya Darasa la Saba na Darasa la Awali ya Shule ya Msingi Elite Dignity, Makongo Juu, jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza umuhimu wa walimu na wazazi kushirikiana katika kutoa malezi, mwongozo na mazingira bora ya kujifunza kwa wanafunzi katika ngazi mbalimbali za elimu.