TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA
(TEWW)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, amehimiza kuanzishwa kwa utaratibu wa kuwaalika wataalamu na wazungumzaji kutoka katika kada na sekta mbalimbali ili kushi
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, amehimiza kuanzishwa kwa utaratibu wa kuwaalika wataalamu na wazungumzaji kutoka katika kada na sekta mbalimbali ili kushi
18th Aug, 2026

Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, amehimiza kuanzishwa kwa utaratibu wa kuwaalika wataalamu na wazungumzaji kutoka katika kada na sekta mbalimbali ili kushirikiana na Taasisi katika kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa ya ziada na kujiimarisha zaidi katika mafunzo ya vitendo.

‎Amesema hayo leo, tarehe 18 Agosti 2026, wakati wa kikao cha wafanyakazi wote wa TEWW kilichofanyika katika Kampasi ya Mwanza, huku watumishi wengine wakishiriki kwa njia ya mtandao kupitia Zoom.

‎Prof. Sanga amesema ushirikiano huo utawapa wanafunzi fursa ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wenye uzoefu wa moja kwa moja katika maeneo yao ya taaluma, hivyo kuunganisha maarifa ya darasani na uhalisia wa mazingira ya kazi. Aidha, amewataka watumishi kuendelea kutekeleza majukumu kwa kuzingatia malengo ya kimkakati ya Taasisi, kutatua changamoto za wanafunzi na wafanyakazi, kuimarisha vikao na mawasiliano ya ndani, pamoja na kubuni miradi mikubwa ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.

slot gacor