Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, amewataka wawezeshaji na wasimamizi wa IPOSA na ZIPOSA kuendelea kutumia teknolojia za kidijitali kwa ubunifu katika kuboresha ujifunzaji na ufundishaji kwa vijana walio Nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu. Amesema matumizi sahihi ya TEHAMA ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la 2023, pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Prof. Sanga ametoa wito huo wakati akifunga mafunzo ya kujenga uwezo wawezeshaji na wasimamizi wa IPOSA na ZIPOSA kuhusu matumizi ya teknolojia ya kidijitali yaliyofanyika katika Kituo cha Elimu Mbadala Unguja, Zanzibar, Julai 24, 2026.