TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA
(TEWW)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
SERIKALI YAWEKA MSUKUMO ELIMU NA UJUZI KWA VIJANA WALIO NJE YA MFUMO RASMI
SERIKALI YAWEKA MSUKUMO ELIMU NA UJUZI KWA VIJANA WALIO NJE YA MFUMO RASMI
22nd Sep, 2026

TANGA, SEPTEMBA 18, 2026 - Serikali imesisitiza dhamira yake ya kuhakikisha vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu wanapata fursa mbadala, jumuishi na nyumbufu za elimu na mafunzo zitakazowawezesha kupata maarifa, ujuzi na stadi za kujiajiri.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi akimwakilisha Waziri ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati wa uzinduzi wa Programu ya Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Shule (IPOSA), inayotekelezwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia KOICA.

Prof. Mushi amesema utekelezaji wa mradi huo umewezesha walimu 100 kupata mafunzo ya Stashahada, walimu 149 mafunzo ya muda mfupi, kujengwa kwa karakana 30 katika mikoa sita na kudahiliwa kwa vijana 2,087 kupitia mfumo wa tuzo ndogondogo za umahiri. Amesisitiza kuwa mafanikio ya programu yanapaswa kuonekana katika mabadiliko ya maisha ya vijana kupitia maarifa, ujuzi, ajira na kujiajiri.

Kwa upande wake, Mkuu wa TEWW, Prof. Philipo Sanga, amesema IPOSA ni sehemu ya juhudi za Serikali za kutoa njia mbadala za elimu kwa vijana ambao hawakupata fursa katika mfumo rasmi au waliokatisha masomo. Amesema programu hiyo inatekelezwa katika mikoa 16, huku awamu inayofadhiliwa na KOICA ikitekelezwa katika mikoa sita, ikiwemo Tanga.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Tanga una Halmashauri sita zinazotekeleza programu hiyo, zikiwa na karakana ya mfano, karakana tano za kawaida na karakana maalum iliyopo Jeshi la Magereza Maweni. Amesema utekelezaji umeimarisha miundombinu ya mafunzo, uwezo wa walimu na mfumo wa mafunzo unaozingatia umahiri

slot gacor