Watu Wazima (TEWW) imezindua wiki tatu za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za utoaji elimu kwa umma kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 17,2025 jijini Dodoma kuhusu maadhimisho hayo ambayo yanatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 25 Agosti,2025 na kufungwa Agosti 27,2025 na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko.
"Maadhimisho haya yenye kauli mbiu isemayo: "Elimu bila ukomo kwa maendeleo endelevu" yanalenga kuhuisha kasi ya wadau wa kitaifa na kimataifa ya kuendeleza elimu ya watu wazima nchini na kuongeza uelewa wa umma kwamba elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi ni nyenzo muhimu kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi", alisema Prof.Mkenda.
Amesema kuwa, maadhimisho hayo yanalenga kuangazia umuhimu mkubwa wa kujua kusoma na kuandika katika kuendelea kujifunza bila ukomo na kuamsha ari na hamasa miongoni mwa vijana na watu wazima ya kupata ujuzi katika masuala ya ujasiriamali na ufundi wa awali.
Vile vile, Prof. Mkenda amesema shughuli mbalimbali ambazo zitafanyika katika wiki tatu hizo kuwa ni mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Magereza wanaoendesha programu za kisomo magerezani na Wakufunzi Wakazi wa TEWW ambayo yatafanyika Julai 28 hadi 30, 2025 jijini Dodoma na yatawahusisha Maafisa Magereza na Wakufunzi Wakazi wa TEWW.
Shughuli zingine ni maonesho ya shughuli na huduma mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima/Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ambayo yatashirikisha taasisi za umma na binafsi na yatafanyika JNICC kuanzia Agosti 24 hadi 27, 2025 pamoja na Kongamano la elimu bila ukomo ambapo wadau mbalimbali wa elimu takriban 1,000 kutoka ndani na nje ya nchi watakutana pamoja kutafakari miaka 50 ya utekelezaji wa dhima na dira ya TEWW na mwelekeo wa elimu bila ukomo.
Ameeleza kuwa, kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa tarehe 25-27 Agosti,2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) ambapo zaidi ya wananchi na wadau 1,000 wa elimu.