TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA
(TEWW)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Vyombo vya habari vimehimizwa kushiriki kikamilifu katika kuandika kuhusu Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi (EWW/ENMR) nchini ili kutoa elimu kwa jamii, kuibua mafanikio na cha
Vyombo vya habari vimehimizwa kushiriki kikamilifu katika kuandika kuhusu Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi (EWW/ENMR) nchini ili kutoa elimu kwa jamii, kuibua mafanikio na cha
08th Sep, 2026

Vyombo vya habari vimehimizwa kushiriki kikamilifu katika kuandika kuhusu Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi (EWW/ENMR) nchini ili kutoa elimu kwa jamii, kuibua mafanikio na changamoto zinazowakabili wananchi, pamoja na kuhamasisha ushiriki katika programu za elimu ya watu wazima.

‎Hayo yameelezwa, Septemba 7, 2026, na Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, wakati akifungua warsha ya kujenga uelewa na kuimarisha ushirikiano kati ya TEWW, vyombo vya habari na wadau katika kuendeleza Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi nchini, iliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la DVV International.

‎Aidha, ameongeza kuwa, wakati nchi ikielekea katika maadhimisho ya Siku ya Kisomo Duniani pamoja na Juma la Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi (EWW/ENMR) mwaka huu, vyombo vya habari vinatarajiwa kuwa na nafasi kubwa katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kisomo na kuendelea kujifunza katika hatua mbalimbali za maisha.

slot gacor