Wanufaika wa programu na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), ikiwemo IPOSA, MUKEJA na SEQUIP-AEP, wakitoa maelezo na ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea Banda la Taasisi hiyo leo, tarehe 23 Septemba 2026, katika Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Kitaifa na Juma la Elimu Bila Ukomo yanayofanyika katika Viwanja vya CCM, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.
Wanufaika hao wameeleza uzoefu wao na namna walivyonufaika na programu hizo kupitia fursa za elimu, maarifa na stadi zinazotolewa na TEWW, huku wakieleza kwa wageni umuhimu wa programu hizo katika kuwawezesha wananchi kujenga uwezo na kuboresha maisha yao. Maadhimisho hayo yanafanyika chini ya kauli mbiu “Kisomo kwa Manufaa ya Watu, Dunia na Ustawi wa Jamii.”