Washiriki wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kidijitali kwa wawezeshaji na wasimamizi wa Mradi wa IPOSA katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Vifaa hivyo vinalenga kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu, pamoja na kuongeza matumizi ya teknolojia katika utoaji wa elimu na stadi za maisha.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo, tarehe 11 Agosti 2026, ambapo vifaa hivyo vimekabidhiwa na Kaimu Naibu Mkuu wa Taasisi – Taaluma, Prof. Sempeho Siafu, kwa niaba ya Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga. Vifaa hivyo vitatumika katika vituo vitatu vya IPOSA ambavyo ni Wailesi, Mzinga na Temeke.