Washiriki wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa wawezeshaji na wasimamizi wa IPOSA na ZIPOSA kuhusu matumizi ya teknolojia ya kidijitali katika kukuza stadi za ujifunzaji na ufundishaji kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu. Mafunzo hayo yanaratibiwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) na yalifunguliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Dkt. Mwanakhamis Adam Ameir, katika Kituo cha Elimu Mbadala Unguja, Zanzibar, tarehe 23 Julai 2026.