Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, yupo nchini Korea Kusini akiambatana na timu ya uratibu wa program ya IPOSA kwa ziara ya mafunzo. Lengo kuu la ziara hiyo ni kupata uzoefu kuhusu uendeshaji wa program za elimu nje ya mfumo rasmi na elimu bila ukomo.
Mafunzo hayo yanatokana na mwaliko wa Shirika la KOICA, mfadhili wa mradi wa IPOSA nchini Tanzania.
Katika hatua nyingine, Prof. Sanga pamoja na ujumbe alioambatana nao walipata fursa ya kumtembelea Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Mhe. Noel Kaganda, ambapo walimkabidhi zawadi za kumbukumbu ikijumuisha vitabu vilivyoandikwa na TEWW.