Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi hiyo mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Kimataifa na Juma la Elimu Bila Ukomo yaliyofanyika tarehe 25 Septemba 2026, Bariadi, mkoani Simiyu. Kulia kwake ni Kaimu Naibu Mkuu wa Taasisi (Utawala), Dkt. Honest Kipasika huku kushoto kwake akiwa Kaimu Naibu Mkuu wa Taasisi (Taaluma), Prof Sempeho Siafu.
KOZI FUPI ZA ELIMU YA WATU WAZIMA 2026/2027 KWA MAAFISA NA WADAU WA ELIMU YA WATU WAZIMA NCHINI
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Sanga (kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Mhe. Noel Kaganda (kulia), mara baada ya kumkabidhi zawadi za kumbukumbu, zikiwemo machapisho mbalimbali ya TEWW, wakati wa ziara ya heshima katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE) ilianzishwa mwaka 1960 kama kitengo cha masomo ya nje ya darasa cha Chuo cha Makerere, chini ya Chuo Kikuu cha London. Mnamo mwaka 1963, Taasisi hiyo iliboreshwa...